FrajuuConnect ni jukwaa linalowawezesha wateja (wanunuzi au wapangaji) kuwasiliana moja kwa moja na wauzaji au wamiliki wa nyumba, viwanja, vyumba, au ofisi.
Tunaunganisha tu - hatuhusiki moja kwa moja na mchakato wa biashara
Tunapenda kuweka wazi kuwa sisi hatufanyi kazi kama wakala wa mali isiyohamishika wala hatuhusiki na makubaliano ya kibiashara kati ya pande mbili. Jukumu letu ni:
Kutoa jukwaa la kuweka na kutafuta matangazo ya nyumba au viwanja.
Kuwezesha mawasiliano kati ya muuzaji/mpangishaji na mteja.
Kuhakikisha kwamba taarifa zinaonekana wazi kwa wote.
Hatuwajibikii kwa mambo yafuatayo:
Ukweli wa taarifa zinazowekwa na watumiaji (wauzaji au wapangishaji).
Malipo au uhamisho wa fedha kati ya pande mbili.
Ubora, hali halisi, au uhalali wa nyumba/kiwanja kinachouzwa au kupangishwa.
Tahadhari kwa Watumiaji:
Tunashauri kila mtumiaji kuhakikisha anafanya uchunguzi wa kutosha kabla ya kufanya malipo yoyote. Kutana na muuzaji ana kwa ana, angalia eneo la mali, na hakikisha kila kitu kiko sahihi.